Jumatatu, 11 Januari 2016

Askari wametumwa nyumba iliyokuwa kuna ugomvi wakafika wakatakiwa kuripoti kwa njia ya simu juu ya walichokikuta

ASKARI: Mkuu tumekuta mama mwenye nyumba kampiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza vibaya sanaa
AFANDE: Kha! kisa mkasa mpk akafanya hivyo
ASKARI: Mama mwenye nyumba alikua anapiga deki mumewe akaingia ndani viatu kabla sakafu haijakauka
AFANDE: Sasa mmesha mkamata huyo mwanamke
ASKARI: Bado mkuu
AFANDE: Kha! sasa mnangoja nini
ASKARI: Si tunangoja sakafu ikauke

.

Msichana alikuwa amekaa na baba yake kibarazani, mara akamuona MVULANA friend wake akija, yule mvulana alipokaribia tu, yule msichana akamwambai:
MSICHANA: Umekuja kuchukua kile kitabu chako, kinachoitwa "DADDY IS AT HOME?" by Ngozi Okafor 
MVULANA: Hapana!, Nimekuja kuazima kitabu cha Maombi kama kinaitwa "WHERE SHOULD I WAIT FOR YOU?" by Ngũgĩ wa Thiong'o
MSICHANA: Aaah! Icho sina ila ninacho kimoja kinaitwa "UNDER THE MANGO TREE" by Chimamanda Adichie 
MVULANA: Ooh! Vizuri, Basi usisahau kuja nacho kesho kitabu cha Okot p'Bitek kile kinachoitwa "CALL ME IN 5 MINUTES BEFORE" Utakapokuja shule.
MSICHANA: Usijali, tena nina kitabu kipya kinaitwa "I WON'T LET YOU DOWN" by Chinua Achebe 
Baba mtu akawatazamaaaa kisha akasema
BABA: Vitabu vyote hivyo, mbona vingi sana, atavisoma vyote kweli 
MSICHANA: Ndio Daddy, huyu mvulana hupo smart sana na ana akili atavisoma vyote hivyo! 
BABA: Sawa! Usisahau kumpatie na kile ambacho nimekiweka pale juu ya meza, kinaitwa "I AM NOT STUPID, I UNDERSTOOD EVERYTHING YOU'VE BEEN SAYING" by Shakespeare! 
Na kuna kingine nimekiweka juu ya kabati la vyombo, kinaitwa "IF YOU GOT PREGNANT PREPARE TO GET MARRIED" by Wole Soyinka.

SWALI LA KIZUSHI


Wewe ni mzazi mwanao anasoma kidato cha tatu mkoani umemsafirisha leo kwenda shule baada ya masaa matano ukasikia gari alilo panda mwanao limepata ajali wamekufa watu wote upo ktk harakati za kuandaa msiba mwanao anakupigia simu baba/mama mimi mzima sijafa mpenzi wangu ABDUL aliniambia nishuke Chalinze ili niwe nae kwa siku mbili alafu niende shule je, wewe mzazi unge mfanyaje mwanao?